Thursday, April 12, 2012

Tiba ya kichwa, kupatwa jini, nguvu za kiume, tumbo lisilopona, kutopata usingizi, n.k

Kila kiungo cha mwanadamu kina kazi mahsusi na ikitokea kiungo chochote kikashindwa kufanya kazi yake basi mwanadamu hukosa raha na amani na kuanza kuangaika kutafuta tiba yake.
Mwenyezi Mungu muumba ndiye aliyeumba mwanadamu na viungo vyake vyote na kuvipangia kanuni ya kufanya kazi kimaumbile, kwa hiyo basi wa kuomba sana pindi tukiumwa ni yeye kwanza na baadaye atatupa mwongozo wa tiba katika kuangaika kutafuta dawa yeye ataamua dawa ipi tupate tupone au tusipone, hii nasema kwa sababu dawa inabidi itumike lakini tukiwa tunajua mwenye kubariki dawa hii ni Mwenyezi Mungu na hapo ndipo yeye ataamua tukapona kwa baraka zake. Ingawa wanadamu tuna jeuri tunapokuwa na afya nzuri na tunajiona kuwa afya yetu tumeimiliki vilivyo na tunasahau hata kusali, kutoa zaka, sadaqa, ila tunazama kwenye machafu kama zinaa, pombe, kamali, n.k. Tunapoumwa tu ndipo wengine tunmuomba Mwenyezi Mungu kwa imani ya kuogopa na akikubali maombi yetu wengine tunarudi huko huko kwenye maasi na hii ni kasumba ya wanadamu kusahau haraka na kufikiri dunia hii wataishi milele na kujidanganya kuwa mtu akifa yameisha hataulizwa kwa yale aliyofanya alipo kuwa hai!!

Kila jema au baya liwe dogo vipi utaulizwa na utalipwa kwayo na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa msamaha basi tubu leo hii na uomb msameaha urudi kwa Mola wako aliyekuumba kutoka katika manii na ukakaa katika kizazi cha mama yako miezi takribani tisa.

Tiba ya nguvu za kiume ni:
Acha zinaa kwanza
Acha sigara kama unavuta
Punguza vyakula vya mafuta
Chukua Habati thufa saga weka ndani ya maziwa fresh moto  kijiko kimoja cha chakula na kunywa mara 2 kwa siku fanya hivyo kwa siku 7
Na kunywa chai yenye mdalasini na tangawizi kila jioni

Kupata usingizi

Fanya Mazoezi ya viungo kama kutembea dakika 15, fyeka uwanja au lima bustanini mpaka uchoke

Kunywa maziwa fresh moto kila jioni

Tumbo lisilopona 

Tafuta sanamaki kiasi cha kujaa viganja viwili

Chemsha maji lita tano

Toa maji kwenye moto na hapo weka viganya viwili vya sanamaki kwenye maji ya moto hayo subiri ipoe na weka kwenye chombo safi na hapo weka asali lita moja na changanya iwe mchanganyiko

Tumia asubuhi na jioni glasi moja moja  na utaharisha kusafisha tumbo, tumia mpaka dawa iishe.

Kuota ndoto za kutisha usiku na watoto kusutuka usingizini

Nunua dawa inayoitwa mvuje(Altiti)

Weka kwenye mafuta kama vaseline na changanya, kila ukitaka kulala jipake mchanganyiko huo

Tuma email: tibaherbs@gmail.com utapewa maelekezo ya tiba

Kuendeleza Blog Hii na kusaidia wenye SHIDA Toa Sadaqa yako ya Hiari na Mungu atakulipa: Tuma MPESA 0764244867. AIR TEL Money 0785883692 

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA